KENANI KIHONGOSI AENDELEA KUWASHA MOTO JIMBO LA NGORONGORO

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi Uvccm Kennani Kihongosi ameendelea na kampeni za kumtafutia kura mgombea ubunge katika Jimbo la Ngorongoro Mkoani Arusha ambapo hii leo amefanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kijiji cha Alailelai. katika Kata ya Alailelai Tarafa ya Ngorongoro.


Akizungumza na wananchi wa kata ya Alailelai amewataka wananchi wa kata hiyo yenye vijiji vitatu kwenda kumchagua kwa kura nyingi kijana wao Emmanuel Ole Shangai ili aweze kuendelea kuchapa kazi na kwa kukamilisha miradi mbalimbali iliyoanzishwa na mtangulizi wake.

"Shangai ana uwezo na uweledi mkubwa katika kuwatumikia wananchi kama alivyokuwa olenasha,Rais samia ameona shangai anatosha kuleta maendeleo hapa ngorongoro na ndio maana amewaletea huyu nendeni mkampe kura zote za ndio ifikapo disemba 11", alisema Kihongosi

"Pia nafahamu hapa kwenye hii kata kuna changamoto mbalimbali ikiwemo za afya,barabara,maji na barabara na mnahitaji fedha za ukwamilishaji wa mabweni mawili katika shule ya msingi kwa sababu watoto wenu huwa wanaliwa na simba wanapoenda shule Rais Samia ameshatoa milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya shule hii lakini pia ameleta milioni 154 kwa ajili ya usambazaji wa maji katika kijiji cha Sendeu",alisema

Kwa upande wake mgombea Ubunge Emmanuel Shangai amesema kuwa, kama atapata ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo, atahakikisha kero zinazowakabili wananchi, zinapatiwa ufumbuzi wa haraka ili waendelea na shughuli za kila siku pasipo vikwazo ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya Kata,ukamilishwaji wa mabweni ya wananfunzi 88 ambayo yote ni viporo yatayogharimu milioni 80 katika shule ya msingi.

“Bado jimbo letu lina changamoto nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa, naombeni kura zenu ili niweze kuwatumikia, nawaahidi katika uongozi wangu, hakuna mwananchi wala mtumishi atakayenyanyaswa na mtu mwingine, nitawatumikia kwa weledi na uaminifu mkubwa" ,Ole Shangai
Na Imma Msumba Loliondo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments