Recent-Post

Madarasa 56 yakabidhiwa Kilimanjaro

Madarasa 56 katika shule za sekondari 36 za Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro yamekabidhiwa kwa mkuu wa Mkoa huo yakiwa tayari kwa ajili ya wanafunzi watakapofungua shule mapema 2022.

 Zaidi ya Sh1.12 bilioni kimetumika katika kutekeleza ujenzi wa madarasa hayo yaliyojengwa  na kukamilika kwa wakati.

Akizungumza leo  Desemba 18, 2021 wakati wa hafla ya kupokea madarasa hayo kwenye Shule ya Sekondari Kibacha , Mkuu wa Wilaya ya Same,  Edward Mpogolo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Stephen Kagaigai amesema madarasa hayo yatakuwa mwarobaini wa kutatua changamoto ya upungufu wa madarasa ndani ya wilaya hiyo.

"Kweli tumepokea madarasa haya kupitia fedha za Covid-19 ambapo sasa ni jukumu letu sisi viongozi na jamii kuwahimiza watoto waweze kusoma kwa bidii huku wakitambua Serikali yao inawajali lakini viongozi wa maeneo husika kuhakikisha miundombinu ya madarasa hayo inalibdwa ipasavyo ili iweze kuwanufaisha watoto wa sasa na vizazi vijavyo," amesema.

Mpogolo ameushukuru Serikali kwa kuwapatia fedha hizo ambazo zimekuja nje ya bajeti na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele kwenye wilaya hiyo.

Yusto Mapende, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo amesema kukamilika kwa madarasa hayo kumeibua hisia kubwa na ari kwa wazazi na walezi katika kuhakikisha watoto wao wanapata elimu na wanafika shuleni kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments