WAZIRI MKUU WA JAMUHURI YA MUNGANO WA TANZANIA MAJALIWA AIPONGEZA UVCCM

Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa akipokea tuzo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Kenani Kihongosi ya kutambua mchango wake na malezi bora kwa Jumuiya na Chama, kwenye fainali wa UVCCM GREEN CUP uliozikutanisha Timu ya mpira wa miguu ya Mkoa wa Magharibi (Zanzibar) na Timu ya mpira wa miguu ya mkoa wa Pwani (Tanzania Bara)  kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, Desemba 12, 2021. (Picha na Uvccm Taifa Di)Dr.Denisi Nyiraha, Gelaidina Kabululu  na Omary Lumoto Wenyeviti Wa Kigoma ,Singida Na Arusha Walio keti Jukwaa Moja Wakiendelea kufatitilia matokeo Mbali Mbali yalikuwa yakiendelea kwenye kilele cha Fainali Za Uvccm TaifaTarehe 12/12 2021

Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa akikabidhi kombe la UVCCM GREEN CUP kwa nahodha wa timu ya Mkoa wa Magharibi Hassan Said Hassan (katikati) na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Magharibi Fahmy Ali (kushoto). Waziri Mkuu alikuwa rasmi katika mchezo wa fainali wa UVCCM GREEN CUP uliozikutanisha Timu ya mpira wa miguu ya Mkoa wa Magharibi (Zanzibar) na Timu ya mpira wa miguu ya mkoa wa Pwani (Tanzania Bara)  kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, Desemba 12, 2021.  (Picha na Uvccm Taifa Dix)

Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa akikagua Timu ya mpira wa miguu ya mkoa wa Pwani (Tanzania Bara) wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Fainali ya UVCCM GREEN CUP uliozikutanisha Timu ya mpira wa miguu ya Mkoa wa Magharibi (Zanzibar) na Timu ya mpira wa miguu ya mkoa wa Pwani (Tanzania Bara)  kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es salam, Desemba 12, 2021.  (Picha na Uvccm Taifa Dix ) Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa Akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi alipokuwa mgeni rasmi katika mchezo wa fainali wa UVCCM GREEN CUP uliozikutanisha Timu ya mpira wa miguu ya Mkoa wa  Magharibi (Zanzibar) na Timu ya mpira wa miguu ya mkoa wa Pwani (Tanzania Bara)  kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam, Desemba 12, 2021. (Picha Na Uvccm Taifa Dix) Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa akikagua timu ya mpira wa miguu ya Mjini Magharibi wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Fainali ya UVCCM GREEN CUP uliozikutanisha Timu ya mpira wa miguu ya Mkoa wa Magharibi (Zanzibar) na Timu ya mpira wa miguu ya mkoa wa Pwani (Tanzania Bara)  kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es salam, Desemba 12, 2021. (Picha na Uvccm Taifa Dix)Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kassim Majaliwa akifuatilia mchezo wa fainali wa UVCCM GREEN CUP uliozikutanisha Timu ya mpira wa miguu ya Mkoa wa Magharibi (Zanzibar) na Timu ya mpira wa miguu ya mkoa wa Pwani (Tanzania Bara)  kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es salam, Desemba 12, 2021. (Picha na Uvcm Taifa Dix)

Asema michuano ya UVCCM GREEN CUP imewaunganisha vijana na kuibua vipaji

Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Kassim Majaliwa ameupongeza Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kwa ubunifu wa kuanzisha michuano ya UVCCM GREEN CUP ambayo imeleta vijana wa Tanzania nzima sehemu moja.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa michezo hiyo ambayo ilishirikisha timu kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa mpira wa miguu na pete itasaidia kuibua vipaji ambavyo vitakuja kuzitumikia timu zetu za Taifa.

Amesema hayo leo Jumapili (Desemba 12, 2021) aliposhuhudia mchezo wa fainali ya mpira wa miguu kati ya Mkoa wa Magharibi (Zanzibar) na Mkoa Pwani (Tanzania Bara) jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu ya Mkoa wa Magharibi iliifunga timu ya Mkoa wa Pwani kwa magoli 3-1

Waziri Mkuu ameushauri Umoja Vijana kuiingiza michezo hiyo kwenye ratiba ya UVCCM taifa ili kila tarehe 9 Desemba ya kila mwaka iwe ni michezo kwa vijana nchi nzima kaunzia ngazi ya wilaya hadi Taifa “lengo ni kuibua vipaji vya vijana wetu na kuwaunganisha”

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi amesema kuwa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi uliona ni muhimu kuanzisha michuano ya UVCCM GREEN CUP kwa ajili ya kuanda na kukuza vipaji vya mpira wa miguu na pete “Lengo lingine la michuano hii ilikuwa pia ni kutunza mazingira na kuimarisha afya”

Kihongosi aliongeza kuwa kupitia michuano hiyo wameweza kukuza umoja, upendo na mshikamano miongoni mwa vijana walioshiriki michuano hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini

Mshindi wa kwanza wa michuano hiyo kwa upande wa mpira wa pete ni mkoa wa Dar es Salaam na nafasi ya pili ilishikwa na Mkoa wa Mjini Magharibi.

Kadhalika, Umoja wa Vijana umekabidhi tuzo Maalumu kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kitambua mchango wake na malezi bora kwa Jumuiya na Chama.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments