MAKAMBO APIGA HAT TRICK, YANGA IKIICHAPA IHEFU FC MABAO 4-0

 


Klabu ya Yanga imefanikiwa kutinga raundi ya nne kombe la shirikisho (FA) mara baada ya kufanikiwa kuwachapa Ihefu Fc mabao 4-0 kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Heritie Makambo ndiye alikuwa mwiba kwa wapinzani katika kipindi cha kwanza alifanikiwa kupachika mabao mawili na bao lingine likifungwa na Khalid Aucho na kwenda mapumziko Yanga ikiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili Yanga ilipinguza kasi ya mchezo mara baada ya kuwapumzisha baadhi ya mastaa wake kadhaa, hivyo baadae Heritie Makambo akapachika tena bao lake la tatu katika mchezo huo na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments