MAKAMU WA RASI AFUNGUA MKUTANO NCHI WANACHAMA WA ZIWA TANGANYIKA


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu amesema manispaa ya Tabora, imetekeleza kwa vitendo agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kutoa mikopo mikubwa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kuwainua kiuchumi.

Waziri Ummy ameeleza hayo leo Alhamisi Desemba 16, 2021 akiwa mkoani Tabora kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na manispaa hiyo, akisema uamuzi wa kutoa mikopo mikubwa utasaidia kuleta tija kwa wana vikundi hivyo.
Katika ziara hiyo, Waziri Ummy ametembelea pia kiwanda cha kuchakata asali cha Miombo Beekiping Initiatives kilichopewa mkopo wa Sh50milioni zilizosaidia kuanzishwa kwa kiwanda hicho, kilichotoa soko la uhakika kwa wafugaji 178.
Waziri Ummy amewapongeza vijana hao kwa kuanzisha kiwanda hicho kitakachoongeza thamani ya asali inayowaongezea kipato, sambamba na kutoa fursa ya soko la uhakika kwa wafugaji wa nyuki.
“Sasa ninyi muwe vijana wa mfano kwa kuhakikisha mkopo huu, mliopewa usio na riba mnaurejesha kwa wakati ili wengine nao wafaidike.Naomba mtafute eneo kubwa nje ya mji ili mjenga kiwanda kikubwa kwa sababu hapa mlipo hapatoshelezi.
“Niwapongeza manispaa ya Tabora kwa kutekeleza agizo hili sina shaka mkopo huu,maeneo mengine wanatoa fedha kidogo ambazo hazileti matokeo,” amesema Waziri  Ummy.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Peter Nyanja amesema katika robo ya kwanza wametoa mikopo yenye thamani ya Sh273.5 milioni katika vikundi 38 wanawake, vinane (vijana) na vinane (watu wenye ulemavu.
Nyanja amefafanua kuwa katika vikundi hivyo, vijana cha Miombo wamekidhi vigezo na kupata mkopo wa Sh200milioni
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Buriani aliyekuwepo kwenye msafara huo, amesema ujenzi wa vyumba vya madarasa  katika halmashauri za Tabora na Nzega umekamilika  kwa asilimia 100 huku  katika halmashauri za Uyui, Urambo, Kaliua na Sikonge ukiwa katika asilimia 90.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments