Recent-Post

Miaka 60 ya Uhuru:Mbali na mazoezi, usafi Kahama Jogging tutachangia damu Hospitali ya Manispaa Desemba 9,2021

ZIMEBAKI siku mbili, sisi Kahama Jogging kufanya jambo letu katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru.

Sisi kwa pamoja tutafanya mazoezi ya viungo na Jogging siku ya tarehe 9 Desemba,2021.

Baada ya hapo kituo chetu cha mwishi kitakuwa Hospitali ya Manispaa Kahama mkoani Shinyanga.

Hapa kila mmoja wetu atakamata fagio na kuhakikisha tunasafisha maeneo yote ya hospitali.

Baada ya hapo sasa sote tutachangia damu kwa pamoja.#NjooTuokoeUhaikwaKuchangiaDamunaKahamaJogging
Ewe mkazi wa Kahama kamilisha Miaka 60 ya Uhuru kwa kuungana na Kahama Jogging tukafanye usafi Kisha tuchangie damu.
 
NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Post a Comment

0 Comments