Recent-Post

MNEC AMSHUKIA SPIKA NDUGAI

Ni Kufuatia Spika Ndugai kubeza hatua ya Serikali kuchukuwa Mkopo usio na masharti.

Ampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumaliza kero ya uhaba wa Madarasa kupitia Mkopo wa Trilioni 1.3 za Uviko 19

                        
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Juma Killimbah amemtaka Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai kumuacha Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kutekeleza ilani ya Chamakatika kuwatumikia watanzania na sio kupiga kelele za kumkatisha tamaa.

Mjumbe huyo ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano na Waandishi wa habari ikiwa Ni siku chache Baada ya Spika Ndugai kubeza hatua ya Rais Samia Kuchukuwa Mkopo nafuu usio na masharti wa Tsh trillion 1.3 kutoka IMF.

Aidha Killimbah amesema Mkopo huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kutatua kero ya uhaba wa Vyumba vya Madarasa na Sasa wanafunzi wanakwenda kusoma pasipo usumbufu wowote.

Hata hivyo Killimbah amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono jitiada zote zinazofanywa na Rais Samia kwakuwa zinalenga kuboresha maisha ya watanzania na kamwe hawatomfumbia macho yoyote anaekwamisha juhudi za Serikali.

Post a Comment

0 Comments