MTATURU JIMBO CUP YAHITIMISHWA RASMI NA WAZIRI WA SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO MHE. INNOCENT BASHUNGWA

Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe Innocent Bashungwa  Tarehe 26/12/2021 Amehitimisha Rasmi Mashindano ya Mpira wa Miguu yaliyojulikana Kama Mtaturu Jimbo Cup Katika Uwanja wa Sekondari Ikungi, Katika Jimbo la Singida Mashariki Wilayani Ikungi mkoani Singida, Ambapo Katika Kuhitkmisha ligi hiyo kulikua na Mechi ya Fainali iliyohusisha timu ya Mampando Fc na Matongo Fc ambambo mechi iliisha kwa Dakika 90 kwa Timu ya Matongo Fc kuibuka  Na Ushindi dhidi ya Mampando Fc.

Waziri Bashungwa ameonyesha kufurahishwa na Taarifa ya Mashindano hayo na kumpongeza mdhamini wa ligi hiyo Mhe. Miraji Mtaturu kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo Jimboni humo.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewataka madiwani kuipa kipaumbele zaidi ajenda ya ujenzi na uboreshaji wa miundo mbinu ya viwanja vya michezo katika halimashauri zao, akisistiza kuwa michezo ni kipaumbele kikubwa kwa jamii, kama ilivyo kwa vipaumbele vingine.

Waziri Bashungwa ametoa wito huo wakati akizungumza katika fainali ya ligi ya Mtaturu Cup iliyofanyika viwanja vya shule ya Sekondari Ikungi mkoani Singida.
        
Amesema Serikali inatamani kuboresha viwanja vyote vya michezo ili viwe na viwango vinavyostahili lakini wakati mchakato ukiendelea ndani ya Serikali ni vyema madiwani kupitia vikao vyao vya halimashauri wakaipa kipaumbele ajenda ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya viwanja vya michezo katika maeneo yao.

Naye Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Jerry Muro ameitumia fursa hiyo kuelezea furaha yake akisema uwepo wa ligi ya Mtaturu Cup umeongeza mwamko wa vijana kushiriki katika michezo na kukuza uhusiano, kutokana na ukweli kuwa michezo ya aina hiyo ni starehe iliyokosekana kwa muda mrefu katika jimbo hilo.


Pamoja na Mambo mengine Waziri Bashungwa Amekabidhi Zawadi kwa Washindi wa Ligi hiyo ambapo
Mshindi wa kwanza amepata
Kombe, Jezi Set 1, Mpira 1 na taslim sh 1,500,000/=
Mshindi wa Pili Mpira 1 na sh 700,000/= Mshindi wa tatu Mpira 1 na Sh 400,000/= Mshindi wa nne
Sh 150,000/= na Mshindi wa tano
Sh 100,000/=
Aidha, Mfungaji bora Amepata Viatu na sh 100,000/= Mchezaji Bora Sh 100,000/= na Golikipa bora
Gloves na sh 100,000/=

Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni Rasmi kuzungumza mbele ya mamia ya wananchi waliofurika uwanjani hapo Mhe Miraji Mtaturu Mbunge Jimbo la Singida Mashariki alimjulisha Mhe. Waziri kuwa ligi hiyo alianzisha kwa lengo la kuwaunganisha vijana na kuibua vipaji Ambapo Ligi ilishirikisha timu 20 toka kwenye kata zote 13 za jimbo hilo na Kumshukuru kwa kuwa Miongoni mwa Mawaziri wasikivu na wanao fikika na kuongeza kuwa Anaishukuru Wizara hiyo kwa kuona Ni Vema Waziri kwenda Kuhitkmisha ligi hiyo.

Mechi Ikiendelea Katika Dimba La Ikungi Secondary 
Washabiki wa Timu zote mbili wakitizama Mechi ikiendelea.
Kwa umahiri Line 2 akiendelea kumsaidia Refa wa Mchezo huo.
Ulinzi ukiimarishwa katika Uwanja wa Mpira Shule ya Sekondari Ikungi.
Ligi ya Mtaturu Cup imehusisha zaidi ya michezo ya 40.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments