NIC Yatoa Msaada Kwa Makundi Maalum

Picha ya pamoja ya kati ya wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na watu wa ulemavu wa viungo na watu wenye ualbino mara baada ya kukabidhi msaada kwa makundi hayo.
Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Karimu Meshack akizungumza mara baada ya kukabidhi vifa kwa watu wenye ulemavu wa viungo na watu wenye ualbino.
Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Karimu Meshack akikabidhi mmoja wa viongozi wa wenye ualbino mafuta kwa jamii hiyo.
Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Karimu Meshack akimsukuma kwenye kiti mwendo mlemavu wa viungo.


*Ni sehemu ya faida ya Shirika kurudisha katika jamii

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) wamekabidhi msaada wa viti vitano kwa watu wenye ulemavu pamoja na mafuta kwa watu wenye ulamavu wa ngozi katika kituo cha Haki Sawa kwa watu wenye ulemavu kilichopo Mabibo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Meneja Mawasiliano wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Karimu Meshack amesema wamefanya utafiti katika kutekeleza sera yao ya kurudisha kwa jamii wakagundua kwamba watu hao wanachangamoto ya vitimwendo na mafuta hivyo wameamua kuwapatia ili waweze kutiimiza majukumu yao.

“Mtanzania ambaye anatembea kwa mikono maana ake kwamba anashindwa kutimiza shughuli zake za kila siku za kiuchumi, anashindwa kutafuta mahitaji yake ya kila siku kwasababu ya mazingira yake ya kutembea”. Amesema Bw.Meshack.

Amesema wenye ulamavu wa ngozi wanahitaji kwenda kwenye majukumu yao lakini mionzi inampa shida katika kutekeleza majukumu yake yya kila siku hivyo basi wamewaleteaa mafuta ili kutatua changamoto zao za afya lakinni wametatua changamoto zao za kujipatia kipato na shughuli za kiuchumi za kila siku.

Ametoa wito kwa taasisi zingine za Serikali pamoja na na taasisi binafsi kuwakumbuka watu wenye ulemavu kwa kutatua changamoto zao za kila siku hasa pale wanapokuwa katika majukumu yao.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kituo Haki sawa cha watu wenye ulamavu Bw.Hilaly Gatunga amesema huduma walizopata kuttoka NIC wamefurahishwa kwa kuweza kuwakumbuka kwa kuwaletea msaada wa vifaa ambavyo vitaweza kuwasaidia kutatua changamoto ziinazowakbili walemavu.

Ameomba baadhi ya makampuni, Taaisisi na mashirika kuwa na moyo wa huruma kwa kuwasiaida watu wenye ulamavu kwa kutatua changamoto zao kwa ujumla.

Pamoja na hayo ameaomba watu wa usalama kujaribu kutoa elimu kwa baadhi ya madereva hasa katika maeneo ya zebra kuweza kuheshimu alama hizo pale wanapopita watu wenye ulemavu wakivuka barabara.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments