Rais wa Somalia amfuta kazi Waziri Mkuu wake, mzozo wapamba moto.

 

  • Rais wa Somalia amfuta kazi Waziri Mkuu wake, mzozo wapamba moto.

Rais wa Somalia amemfuta kazi Waziri Mkuu wake wakati huu wa kuendelea uchaguzi wa bunge na hivyo kuzusha mzozo mpya wa kisiasa katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Vyombo vya habari vimeripoti habari hiyo na kusema kuwa, Rais Mohamed Abdullahi Farmaajo alichukua hatua hiyo jana Jumapili akimtuhumu Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble kuwa anahusika na ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma.

Hatua ya kufutwa kazi ghafla Waziri Mkuu wa Somalia imechukuliwa na rais wa nchi hiyo katika hali ambayo kwa muda sasa wanasiasa hao wawili wana mzozo kuhusu uchaguzi wa bunge na wamefikia hata kulumbana hadharani. 

Baada ya kufutwa kazi, Roble amesema, jambo hilo halitomzuia kuendelea na kazi zake zake za uchaguzi bali atafanya shughuli zake hizo kwa kasi kubwa zaidi.

Jana Jumapili, wanasiasa hao wawili walizozana hadharani huku kila mmoja akimshutumu mwenzake kwa kufanya uzembe na kutotekeleza ipasavyo majukumu yake.

Uchaguzi nchini Somalia

 

Baada ya hatua hiyo ya Rais wa Somalia ya kumfuta kazi Waziri Mkuu wake, sasa nafasi hiyo itabakia wazi hadi uchunguzi utakapokamilika kuhusu shutuma za ufisadi zilizotolewa dhidi ya Roble.

Akitangaza kumfuta kazi Waziri Mkuu wake, Rais Farmaajo amesema, aliyefutwa kazi ni Waziri Mkuu tu na kwamba Baraza la Mawaziri halijavunjwa na mawaziri wataendelea na shughuli zao kama kawaida kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi hiyo.

Uchaguzi wa bunge la Somalia ulianza tarehe Mosi mwezi uliopita wa Novemba na ulipangwa kumalizika tarehe 24 mwezi huu. Hata hivyo mbunge mmoja amesema, hadi wakati huo ni wabunge 24 waliokuwa wamechaguliwa kati ya wabunge 275 wanaopaswa kwenda Bungeni. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments