RC SENDIGA AMERIDHIRISHWA NA UJENZI WA MADARASA YA UVIKO 19 IRINGA DC

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Iringa na wakandarasi wakati wa ziara ya kukagua miradi ya kimaendeleo katika halmashauri ya wialaya ya Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Iringa na wakandarasi wakati wa ziara ya kukagua miradi ya kimaendeleo katika halmashauri ya wialaya ya Iringa
Moja kati ya madaraja ambayo yanaendelea kujengwa katika barabara za halmashauri ya wilaya ya Iringa.

Moja kati ya madaraja ya watembea kwa miguu ambayo yanaendelea kujengwa katika barabara za halmashauri ya wilaya ya Iringa.



Na Fredy Mgunda,Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga ameridhirishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Uviko 19 na kuziagiza Halmashauri zote kuhakikisha miradi yote mipya ya ujenzi wa majengo inakamilisha ndani ya siku 60 pekee

Akiwa katika Ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa, Halmashauri ya Wilayani ya Iringa Sendiga alisema kuwa kasi ya ujenzi wa vyumba hivyo iwe chachu kwa Halmashauri na wakandarasi kukamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati.

RC Sendiga aliupongeza uongozi wa wilaya ya Iringa na Halmashauri ya Iringa kwa kusimamia vilivyo hadi kukamilisha kwa wakati miradi hhiyo ya ujenzi wa madarasa ya fedha za UVIKO 9.

Alisema kuwa madarasa hayo yamekamilika kila kitu kilichobaki ni kuwasubili tu wanafunzi waanze kuyatumia kipindi ambacho watakuwa wanaanza mwaka wa masomo.

ziara hii ya mkuu wa mkoa wa Iringa imejiri ikiwa ni Wiki Kadhaa zimesalia kabla ya muda uliotolewa na Serikali kukamilishwa kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa yanayojengwa kwa msaada wa fedha za uviko 19

Alisema kuwa amefurahishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa huku akiwahakikishia wananchi kuwa vyumba hivyo vitakamilika kwa wakati na viutatumika kwa masomo hapo mwakani

Katika Ziara hiyo Mkuu huyo wa mkoa pia amekagua ujenzi wa miundombinu ya Barabara na madaraja na kutoa muda wa wiki mbili kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wa daraja la Tosamaganga kabla ofisi yake haijamchukulia hatua.

RC Sendiga alisema kuwa hafurahishwi hata kidogo na kasi ya ujenzi wa daraja la Tosamaganga kwa kuwa mkandarasi wa daraja hilo yupo nje ya mkataba nab ado hajakamili ujenzi na kupelekea adha kubwa kwa wananchi ambao wamekuwa wanalitumia daraja hilo.

Aidha Sendiga pia amekagua ujenzi wa barabara pamoja na daraja la lilopo katika barabara ifunda, bandabinchi linalogharimu zaidi ya milioni 984 ambapo amelidhishwa na ujenzi wa daraja hilo pamoja na barabara hiyo.

Alitumia muda huo kumpongeza injinia wa Wakala wa barabara mjini na Vijijini Wilayani Iringa Barnaba Jabiry kwa kazi nzuri ya usimamizi wa daraja na barabara hiyo.

Kwa upande wake Injiania wa Wakala wa barabara mjini na Vijijini Wilayani Iringa Barnaba Jabiry amelitaja daraja hilo kuwa mkombozi kwa wakazi wa kata takribani 3 wilayani humo.

Alisema kuwa daraja hilo likikamilika litakuwa mkombozi wa shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa kata hizo tatu za Tarafa ya Kiponzero na nje ya Tarafa hiyo kwa kukuza maendeleo

Naye mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa wamefanya kazi kubwa kuhakikisha miradi ya madarasa ya fedha za UVIKO 19 yanakamika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa kitaifa na kimataifa.

Alisema kuwa mkurugenzi na wataalam wake wamekuwa hawapumziki kila uchwao wapo barabrani kuhakikisha miradi ya ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati kama ulivyokuwa umepangwa.

Moyo alisema watendaji hao wamefanya kazi kubwa ya kusimamia miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika Halmashuri hiyo na hawapaswi kuvunjwa mioyo yao kwa kuwakatisha tama wakati wa usimamizi wa miradi hiyo.

Mbunge wa jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga alisema kuwa anaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha za kutekeleza ujenzi wa miradi ya barabara na madaraja katika jimbo hilo ambalo awali kulikuwa kuna kero nyingi kwa wananchi juu ya daraja hilo ambalo litatumiwa na zaidi ya kata tatu za Tarafa ya Kiponzero.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments