Sababu Samia kuitenga wizara ya maendeleo jamii kutoka wizara ya afya

Rais Samia Suluhu Hassan amesema uamuzi wake wa kuitenga wizara itakayoshughulikia jinsia, maendeleo,  wanawake na wizara ya afya  ni kuimarisha utekelezaji wa mipango na sera.

Ameeleza hayo  leo Alhamisi Desemba 16, 2021 katika uzinduzi wa kamati ya ushauri ya kitaifa kuhusu utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye jukwaa la kizazi chenye usawa katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Dodoma.

Sasa ndugu zangu unaweza kuona kwamba pamoja na jitihada zote tulizozifanya na mipangano na sera zote tulizoweka bado hatujafika tulipotakiwa kufika."

Sasa ili tuweze kufika tunapotakiwa kufika lazima kuwe na usimamizi, uratibu, kutathimini na ufuatiliaji wa sera na utekelezaji wetu wa mipango. Wizara hizi mbili mkizitizama ni afya na..., uamuzi wangu ni kuitenga wizara itakayoshughulikia jinsia maendeleo wanawake na mambo mengine," amesema.

Huku akishangiliwa amesema, "kutoka kwenye kuchanganywa na wizara ya afya kwa sababu tukiweka wizara ya afya na mambo mengine na  hali tuliyonayo sasa duniani sekta ya afya pekee yake inachukua sura kubwa ya wizara hii kuliko vipengele vingine vilivyobaki.

Lakini kama tutatenga vipengelee vingine vilivyobaki na afya tukaisimamisha pekee yake usimamisizi wa sera, sheria na mambo mengine unaweza ukaenda vizuri na ukapata msukumo unaohitajika. Kwa hiyo hayo ndio maamuzi yangu na nitajaribu kumshawishi Rais wa Zanzibar naye afanye hivyo hivyo ili twende vizuri.”

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments