Recent-Post

SARA BANKS KUWAINUA WAKINA MAMA KIUCHUMI MKOANI ARUSHA

 
(Mratibu Wa Mradi Wa Kuwainua Wanawake Kiuchumi Mkoani Arusha) Bi Mesha Pius Singolyo 
            
Mradi huu unajishghulisha na kuwajengea wanawake uwezo na kuwapa mitaji ya kuanzisha biashara ya pamoja ambayo wakinamama wenywe huchangia nusu ya mtaji na mradi unawaongezea nusu iliyobaki. 

(Mratibu Wa Mradi Wa Kuwainua Wanawake Kiuchumi Mkoani Arusha) Bi Mesha Singolyo

Hivyo Wakinamama huchangia M.3 na Sara naye huwapa 3M jumla zinakuwa 6 na wananunua ngombe Na Kuwanenepesha kwa miezi kadhaaa kisha kuwauza na kugawana faida, Fedha hizo ni ruzuku  na sio deni wao kazi yao ni kula faida na kuzungusha mtaji.

Mratibu Mradi Wa Kuwainua Wakinamama Mkoani Arusha Bi Mesha Pius Singolyo ni mratibu wa mradi huu , Ambao katika kufunga mwaka 2021 wamefanya hafla fupi wilaya ya Monduli na kugawa 12 M kwa vikundi 4 vya wamama.


Mgeni Rasmi Mkuu Wa Wilaya Ya Monduli Akikabidhi Vikundi Pesa 

Baadhi Ya Wanakikundi Wakibudisha Mbele ya Mgeni Rasmi

Pia  Bi Mesha Singolyo  Amesema Anategemea Kufika Wilaya Ngorongoro week Ijayo Ambapo Atagawa Milioni 9 Kwa Vikundi 3 Kata Ya Orbomba, Digodigo Na Sale.

Baada Ya Kupatiwa  Pesa Vikundi Hivyo Huelekea Sokoni(Minadani) Kwajili Ya Kujipatia Ngombe Kwajili Ya Kuwaborsha na kuwa Fanyia Biaashara Ilikujiongezea Kipato Katika Vikundi Vyao

Post a Comment

0 Comments