Serikali yatoa tahadhari Uviko-19

Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa tahadhari kwa wananchi kuzingatia kujikinga na Uviko-19 na kwamba ugonjwa huo bado upo hivyo huenda maambukizi yakaongezeka.

Aidha katika kuelekea msimu huu wa sikukuu wananchi wametakiwa kufuata miongozo ya kujikinga na ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi Desemba 18, 2021 na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifelo Sichwale katika tamko rasmi alilolitoa kuhusu kuongezeka kwa visa vya mafua nchini.Nawakumbusha kuwa ugonjwa wa Uviko-19 bado upo na huenda maambukizi ya ugonjwa huu yakaongezeka hasa tunapoelekea mwisho wa mwaka unaohusisha kipindi cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Hivyo, vema tuzingatie kuchukua tahadhari zote kama zinavyoelimishwa na wataalamu wa afya bila kusahau kuchanja,” amesema Dk Sichwale.

Ameagiza kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima, kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuhakikisha kuwa kila mtu anapata dozi kamili ya chanjo.

Aidha kufuatia kuenea kwa ugonjwa wa mafua amewataka wananchi kutoa taarifa za tetesi za viashiria vya magonjwa ya mlipuko kutoka katika jamii kupitia namba ya simu 199 bila malipo yoyote.

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, kumekuwa na taarifa zenye kuonyesha kuwa watu wengi wana dalili za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka.

Dk Aifelo amesema Wizara imefuatilia na kubaini kweli kuna ongezeko la wananchi kupata dalili za mafua.

Hata hivyo, hii huwa ni hali ya kawaida kila mwaka (seasonal influenza) ambayo huchangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa kama ambavyo iliweza kushuhudiwa kwa miaka mingine iliyopita.

Wizara na taasisi zake tunaendelea kufuatilia kwa karibu viashiria vya mwenendo wa hali hii. Aidha, Wizara inashauri kuwa wananchi wenye dalili hizi za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka watoe taarifa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wafanyiwe uchunguzi wa kitaalamu na wapatiwe matibabu stahiki,” amesema Dk Aifelo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments