SIMBA SC ILEEEE! MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

 WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC wamefuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup) msimu wa 2021-2022 baada ya ushindi wa jumla wa mabao 4-2 dhidi ya Red Arrows ya Zambia katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Mashujaa mjini Lusaka nchini Zambia.

Simba SC licha ya kucheza chini ya kiwango katika mchezo huo ilipokea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa wenyeji Red Arrows katika mchezo huo wa mkondo wa pili. Simba SC walipata ushindi wa bao 3-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wiki moja iliyopita nyumbani Banjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania.

Katika mchezo huo, wa pili Red Arrows walipata mabao yao mawili kupitia kwa Wachezaji Ricky Banda na Sadam Phiri wakati bao la Hassan Dilunga likiwakatisha tamaa kabisa Red Arrows katika mchezo huo.

Simba SC wanafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika badala ya kushindwa kufuzu hatua hiyo kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) siku chache baada ya kutupwa nje na Klabu ya Jwaneng Galaxy FC ya Botswana wakati nyumbani Tanzania.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments