UFUGAJI WA KIBIASHARA NI JAWABU LA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA NCHINI-ULEGA


NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akizungumza mara baada ya kutembelea Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) kilichopo Kongwa leo Desemba 15,2021.


NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI), Dkt. Daniel Komwihangilo mara baada ya kutembelea Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) kilichopo Kongwa leo Desemba 15,2021.


NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mfawidh wa Kituo cha Utafiti Mifugo Kongwa, Salum Kuwi baada ya kutembelea Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) kilichopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2021.


NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akizungumza na viongozi wa Kituo Atamizi cha KilimoBiashara kwa vijana cha PASS-AIC kilichopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2021 mara baada ya kutembelea kituo hicho.


Mkurugenzi wa PASS-AIC, Tamimu Amijee,akitoa taarifa fupi ya Kituo Atamizi cha KilimoBiashara kwa vijana cha PASS-AIC kilichopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2021 baada ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kutembelea kituo hicho.


Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti na Mafunzo Dkt.Hassan Mruttu,akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega katika Kituo Atamizi cha KilimoBiashara kwa vijana cha PASS-AIC kilichopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2021.

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akiendelea kukagua na kujionea maendeleo ya Kituo Atamizi cha KilimoBiashara kwa vijana cha PASS-AIC kilichopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2021.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akitoa maelezo wakati wa ziara ya kukagua Kituo Atamizi cha KilimoBiashara kwa vijana cha PASS-AIC kilichopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2021.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remidius Emmanuel wakati akitoa maelezo katika ziara ya kukagua Kituo Atamizi cha KilimoBiashara kwa vijana cha PASS-AIC kilichopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2021.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa PASS-AIC, Tamimu Amijee mara baada ya kukagua Kituo Atamizi cha KilimoBiashara kwa vijana cha PASS-AIC kilichopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2021.


Muonekano wa banda linalohifadhi mbuzi katika Kituo Atamizi cha KilimoBiashara kwa vijana cha PASS-AIC kilichopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2021.

................................................................

Na Alex Sonna, Kongwa

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema ufugaji wa kibiashara ni jawabu la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini.

Ulega ameyasema hayo leo wilayani Kongwa alipokuwa akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) na Taasisi ya PASS Trust baada ya kutembelea Kituo cha Taliri Kongwa na Kituo atamizi cha kilimobiashara kwa vijana cha PASS-AIC.

Amesema ufugaji na uvuvi wa kibiashara na kisasa ni suluhisho kubwa katika ajira kwa vijana.

“Pia itasaidia nchi katika kuongeza kipato lakini vile vile kuwasaidia watu kutokana na hali duni, kwa hiyo kazi tunayoifanya hapa ya uatamizi ni kutengeneza wafanyabishara wa mifugo wa kisasa.”

“Tunanenepesha mbuzi ambao wanaingia sokoni na kazi hii tumeianza hapa Kongwa na tunatamani iende sehemu nyingi sana na wengine tunawakaribisha waje wajifunze hapa Halmashauri zitakazopendezwa na mradi huu waingize kwenye maeneo yao ili kutoa ajira zaidi kwa vijana wetu,”amesema.

Amesema serikali itawasaidia kupata maeneo vijana watakaovutiwa na kazi hiyo.

“Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwasasa tutawapa ardhi wale wanaokwenda kufuga na si kuchunga, pia serikali yetu imefungua milango ya kibiashara tuna viwanda viwili vikubwa vya nyama na mahitaji ni makubwa,”amesema.

Ulega amesema kwenye uvuvi yanaenda kufanywa mapinduzi makubwa kulingana na matakwa ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

“Tunafufua shirika letu la Uvivu la Tafico litafanya ubia na makampuni yanayoweza kufanya ubia nayo yenye mitaji mikubwa ya kibiashara kwa lengo la kukuza sekta na kuwaondoa wavuvi wetu kwenye matumizi ya vyombo duni,”amesema.

Ameongeza “Serikali ya Mama Samia imenunua mitambo mingi kwa hiyo tutachimba mabwawa na malambo kwenye maeneo yenye ukame ni maeneo ambayo yatakuwa yamekatwa kwa ajili ya wafugaji, na mfugaji atakayepekwa pale tutakuwa tumemtambua na idadi ya mifugo yake.”

Naibu Waziri huyo amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha wanapata mikopo ya kuboresha ufugaji wao na vijana wengi kujiingiza kwenye shughuli hiyo.

“Sekta ya mifugo na uvuvi ni sekta za kibiashara tunataka vijana zaidi waingie huko wakazalishe na kujenga taifa letu,”amesema.

Akitoa taarifa ya kituo atamizi,Mkurugenzi wa PASS-AIC, Tamimu Amijee, amesema kwa kipindi cha miaka miwili ya kituo hicho zaidi ya mbuzi 2500 wa kienyeji wamenunuliwa na PASS kutoka kwa wafugaji katika maeneo tofauti kwa ajili ya vijana ambao wanaendesha biashara hiyo ya unenepeshaji wa mbuzi.

Amesema kuna tatizo la upatikanaji wa mitaji kwa vijana kwa ajili ya kilimobiashara kutokana na kuwepo na dhana kuwa vijana hawakopesheki.

“Kuna changamoto ya vijana kupata maeneo kwa ajili ya kilimobiashara, maeneo yaliyorasmishwa hayapatikani kwa urahisi au hayapo kabisa kwa sehemu nyingi ya nchi, na kama yapo basi yamekuwa nje ya uwezo wa vijana kuyamudu,”amesema.

Hata hivyo amesema mipango ya mwaka 2022/23 kituo kinategemea kuongeza idadi ya vijana kutoka 20 hadi 50.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remidius Emmanuel, amesema Wilaya hiyo imekuwa ikishirikiana na taasisi hizo ili kuleta matokeo chanya na kuinua uchumi kwa wananchi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments