Ukame wasababisha mifugo kupewa unga Simanjiro


 Hali ya ukame uliopo Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imesababisha mifugo kukosa majani ya malisho na kusababisha wengine kupewa unga.

  

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Baraka Kanunga ameyasema hayo mjini Babati kwenye kikao cha Ushauri cha Mkoa huo (RCC).

Kanunga amesema kutokana na hali hiyo wafugaji wanaomba waruhusiwe waingize mifugo yao pembezoni mwa pori tengefu la Mkungunero.

"Wafugaji wa Wilaya ya Simanjiro wamekumbwa na wakati mgumu kweli kweli na mifugo ndiyo benki zao tunaomba waruhusiwe kuingiza mifugo yao pembezoni mwa Mkungunero," amesema Kanunga.

Amesema kutokana na ukosefu wa malisho baadhi ya mifugo inapewa unga ili ile kupambana na njaa badala ya kula majani.

Mbunge wa Vijana Taifa kupitia Mkoa wa Manyara, Asia Halamga amesema hali ni ngumu kwa wafugaji wa wilaya za Simanjiro na Kiteto.

"Wafugaji na wakulima wa Simanjiro na Kiteto wana hali ngumu mno hivi sasa kutokana na ukame kwani wanategemea kuendesha maisha yao kwa kilimo na ufungaji," amesema Halamga.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa mkoa huo, Charles Makongoro Nyerere ameahidi kutembelea eneo hilo ili kushuhudia hali hiyo.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments