Recent-Post

Waandishi Wa Habari Nchini Watakiwa Kuandaa Habari Zenye Utafiti

Mkufunzi kutoka Tasisi ya a Utafiti Repoa, Profesa Pascal Mihyo akizungumza na Wahariri na Waandishi waandamizi kutoka Vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati wa Mafunzo yaliyoandaliwa na Repoa Kwa siku Mbili. 

Afisa Habari kutoka Tasisi ya Utafiti Repoa Godfrey Kalagho akizungumza jambo mbele ya Waandishi wa habari waandamizi na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya habari.
Mkurungezi Mkuu wa Repoa ,Dr.Donald Mmari akizungumza na Waandishi wa habari.

Na Mwandishiwetu
WAANDISHI wa habari nchini watakiwa kuandaa habari zenye utafiti kwa kutumia uandishi wao ili wananchi wafikiwe na habari zilizochakatwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya tafiti na kupunguza umaskini, (REPOA) Dkt. Dornald Mmari amewataka waandishi kuongeza ufanisi katika kuchakata habari.

Alisema REPOA inatambua mchango na umuhimu wa waandishi wa habari na inaamini kuwa waandishi ndio wanauwezo mkubwa wa kujenga au kupomoa katika jamii.

"Waandishi wa habari tunawatengeneza ili kuweza kubadilisha fikira mbaya kwa watanzania, waandishi wanatakiwa kuandika habari zenye tafiti ili Kuweza kuwasaidia wananchi kupata habari zilizo chakatwa vizuri."alisema Dkt. Mmari

Aidha alitoa mfano wa mauaji ya kimbali yaliotokea mwaka 1994 na kubainisha kwamba vyombo vya habari ndivyo vilichochea mauaji hayo.

"Mnachokiandika mnatakiwa kuwa makini kwa kuwa mnauwezo wa kuaminisha watu na wakaamini na kuchukua nafasi kubwa juu ya mnachokiandika katika habari."

Mfano mnapoafika juu ya mradi fulani ulioshindwa kuendelea mnatakiwa kujikita na ulianzia wapi, chimbuko lake ni nini na nini kimefanya hadi umekwama, mnaweza kujikita na taasisi za utafiti ilikupata taarifa iliyoshiba zaidi."alisema Dkt. Mmari.

Aliongeza kuwa semina hiyo kama watafiti kunaona namna ya kuwafikia wananchi kupitia waandishi wa habari.

Alisema Mafunzo hayo wanayatoa kwa watu mbalimbali ikiwemo, Wabunge na watumishi wa umma na tutaendelea kuyatoa.

Post a Comment

0 Comments