Wakimbizi nchini Uganda waishukuru UN kwa ulinzi na huduma zake kwao mwaka 2021

 

  • Wakimbizi nchini Uganda waishukuru UN kwa ulinzi na huduma zake kwao mwaka 2021

Tukiwa tumekaribia mno kuingia katika mwaka mpya wa 2022 wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali wilaya ya Hoima nchini Uganda wametoa shukrani zao kwa Umoja wa Mataifa na wakati huo huo wameomba kusaidiwa zaidi mwaka ujao hasa wakati huu ambapo bado kuna changamoto za kimaisha zinazosababishwa na janga la ugonjwa wa corona au UVIKO-19.

Miongoni mwa wakimbizi hao ni Benjamini Basebanya ambaye anazungumzia changamoto aNAzokumbana nazo akisema, “unajua shule zimefungwa, hakuna pesa na watu hawafanyi kazi kwa kuwa wamezuiwa kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19. Mipango ilikuwa mingi, tulikuwa tunajaribu kupata elimu zaidi, lakini shule zimefungwa. Amesema, tangazo la serikali ya kwamba shule zitafunguliwa mwaka ujao ni mpango mzuri kwa kuwa wakati huu wa kufungwa shule baadhi ya vijana wameharibika na kutumbukia kwenye ulevi.

Mkimbizi huo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia amesema: “Kifedha tuko chini sana kutokana na UVIKO-19 lakini tuko tayari kurejea shuleni. Unajua kutokuwepo shuleni kuna lazima wasichana waoelewe wakiwa bado wadogo, wavulana wadogo nao wanaoa na miaka miwili wamepoteza bila ya masomo, hivyo wanaona huu ndio mwisho wa maisha.” 

Wahanga wakubwa wa janga la ukimbizi ni wanawake na watoto wadogo

 

Mkimbizi mwingine wa Kongo DR aliyeko kwenye kambi ya wakimbizi ya Kyangwali huko Hoima, Uganda, ni Faraja Lanem wa aliyetokea kijiji cha Kasonga ambaye amesema “mwaka 2021 tumepata shida ya UVIKO-19 lakini tumepata ulinzi kutoka UNHCR kwani walitupatia chanjo. Tunashukuru sana. Shida sasa wakati wa Corona ni uhaba wa chakula, mashamba hatuna tena na hata fedha tumepunguziwa.”

Tabu Mawazo naye ni mkimbizi wa DRC anayeishi kwenye kambi hiyo. Anasema, “jinsi mimi niko hapa nafanya biashara, nakuwa makini na hii UVIKO-19 kwa kuwa huwezi tu kukaa nyumbani ukisema unaogopa utapata corona. Mimi nashukuru Mungu jinsi ananipitisha kwenye hii UVIKO-19 na mimi najua hii miaka inakuja miaka itakuwa vizuri kwa kuwa wametupatia chanjo.”

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments