WANADODOMA WATAKIWA KUIUNGA MKONO DODOMA JIJI FOOTBALL CLUB

 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh.Jabir Shekimweri amewataka wananchi na wadau wa michezo Jijini Dodoma kuiunga mkono kwa hali na mali Timu ya Dodoma Jiji ya Mkoani hapo.


Mh. Shekimweri ameyasema hayo leo wakati akipokea basi jipya Timu ya Dodoma Jiji katika uwanja wa Jamhuri na kuchukua fursa hiyo kutoa rai kwa wanaDodoma kuwa mstari wa mbele kuipigania timu yao.

“Timu hii ndio utambulisho wetu,kila mwanaDodoma lazima ajivunie uwepo wake na hivyo kuisaidia Timu yetu iendelee kufanya vizuri.

Tuna timu bora,nzuri na tishio ambayo Wana Dodoma tukiendelea kuiunga mkono itafika mbali na kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh.Anthony Mavunde amewashukuru wadau wote walioshiriki katika mchakato wa upatikanaji wa basi hilo jipya la Timu na kuahidi kuendelea kutafuta wadau wengi zaidi wa Dodoma na nje ya Dodoma kuisaidia Timu na kwa sasa wapo katika mazungumzo na Kampuni mbili kubwa moja ya Maji na nyingine ya Vifaa vya Ujenzi ili kuona kama wanaweza kupata ufadhili wa Timu hiyo.

Akishukuru kwa niaba ya wachezaji,Kapteni wa Timu ya Dodoma Jiji FC Mbwana Kibacha amewashukuru viongozi wa Timu na wadau wengine kwa kutimiza ahadi yao ya kuwatafutia usafiri mzuri na kuahidi kwamba watajitahidi kufanya vizuri katika michezo inayofuatia ili kuendelea kulinda heshima ya Dodoma.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments