Waziri wa Nchi ofisi Ya Rais tamisemi Mhe. Ummy Mwalimu ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Singida kwa kukutana na Sekretarieti ya Mkoa wa Singida na kupokea taaarifa ya mkoa, kujadili hali ya watumishi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na upelekaji wa fedha za mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo.
Katika kikao hicho kwa pamoja wamekubalina namna bora ya Utekelezaji wa shughuli za Serikali katika Mkoa wa Singida.
0 Comments