Recent-Post

YANGA YAIADHIBU TANZANIA PRISON MABAO 2-1

Klabu ya Yanga imendelea kusalia kileleni mara baada ya kufanikiwa kuwachapa Tanzania Prison mabao 2-1 kwenye uwanja wa Nelson Mandela wilayani Sumbawanga.

Mabao ya Yanga yalifungwa na nyota wao Feisal Salumu dakika ya 23 pamoja na Khalid Aucho ambaye alifunga dakika ya 44 kipindi cha kwanza.

Tanznaia Prison ndo walianza kutangulia kwa bao la mapema kabisa lililofungwa na Mbagula dakika ya 12 ya mchezo kipindi cha kwanza.

Katika msimamo mpaka sasa Yanga anaongoza akiwa na pointi 23 akifuatiwa na mahasimu wao Simba Sc wenye pointi 18 wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
NA EMMANUEL MBATILO

Post a Comment

0 Comments