Afrika yalalamikia kupokea chanjo za corona zinazokaribia kupitwa na wakati

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika CDC kimesema kuna udharura wa kupelekwa barani humo chanjo za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 ambazo muda wake wa matumizi ni baina ya miezi mitatu hadi sita.

Mkuu wa kituo hicho cha Umoja wa Afrika, John Nkengasong amesema hayo leo Alkhamisi na kufafanua kuwa, bara hilo limepokea mamilioni ya dozi ambazo muda wake wa matumizi unaelekea kumalizika.

Afisa huyo wa Afrika CDC ameeleza bayana kuwa, kufikia sasa dozi milioni 2.8 za chanjo zilizopelekwa katika nchi za bara hilo zimepitwa na wakati.

Dakta Nkengasong ameeleza bayana kuwa, ingawaje dozi hizo ni sawa na asilimia 0.5 tu ya dozi milioni 572 zilizopelekwa barani humo kufikia sasa, lakini zingeweza kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.

Hivi karibuni, serikali ya Uganda ilitangaza habari ya kuteketeza dozi laki nne za chanjo za corona, ambazo muda wake wa matumizi ulikuwa umepita.

 

Mkuu wa Afrika CDC, John Nkengasong

Wakati huohuo, Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani barani Afrika amekosoa hatua ya nchi tajiri duniani kujirundikia chanjo za corona bila kuzijali nchi masikini.

WHO inasisitiza kuwa, ingawaje maambukizi ya virusi vya corona yamepungua sana, lakini ipo haja kubwa sana ya kuendelea kutoa chanjo kwa watu.

Nchi nyingi hasa barani Afrika zinategemea msaada wa chanjo kutoka kwa mpango wa COVAX wa Umoja wa Mataifa wa kugawa chanjo bila malipo kwa nchi masikini. Nchi tajiri duniani zinalaumiwa kwa kutochangia chanjo kupitia mpango huo wa COVAX, mbali na kuhodhi chanjo zenyewe. 


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments