Baada ya miezi saba, hatimaye serikali ya Nigeria marufuku ya twitter

Serikali ya Nigeria ilisimamisha matumizi ya mtandao wa twitter Juni mwaka jana (2021) baada ya kampuni hiyo kufuta ujumbe wa Twitter wa Rais Muhammadu Buhari kuhusu kuwaadhibu wanaotaka kujitenga nchini humo.

Mamlaka zilishutumu kampuni hiyo kwa kuegemea upande wa watu wanaotaka kujitenga.

Lakini serikali ilisema inabadilisha marufuku hiyo baada ya twitter kukubaliana na masharti ikiwa ni pamoja na kufungua ofisi yake ndani ya Nigeria.

Hatua hiyo inaruhusu mamilioni ya watu katika taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika kutumia mtandao huo tena.


 Baadhi ya watumiaji walikuwa wameendelea kufikia tovuti hiyo baada ya kusimamishwa kwa kutumia VPN, lakini serikali iliapa kuwabana wale ambao bado wanatuma ujumbe kwenye Twitter  ikiwa ni pamoja na mashirika ya vyombo vya habari. Hatua ya mwaka jana ya serikali ya Nigeria ilizua malalamiko ya kimataifa kuhusu uhuru wa kujieleza.

Serikali ilikuwa imeamuru watoa huduma za mtandao kuzuia Twitter, kwa madai kuwa ilikuwa inatumiwa kudhoofisha "uwepo wa Nigeria kama nchi" kupitia kueneza habari za uongo ambazo zinaweza kuwa na "madhara ya vurugu".

Twitter ni maarufu kwa Wanigeria wengi, na jukwaa hilo limetumika kama zana ya kuhamasisha. Wanaharakati waliitumia kutafuta uungwaji mkono wakati wa maandamano dhidi ya ukatili wa polisi chini ya alama ya reli #EndSars, ambayo ilivutia watu duniani kote.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments