Biashara ya Kenya na Tanzania yaimarika kufuatia agizo la Rais Samia

  • Biashara baina ya Kenya na Tanzania inazidi kuimarika miezi kadhaa baada ya kuja madarakani Rais Samia Suluhu Hassan nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Idara ya Takwimu Kenya, kuanzia Januari hadi Septemba 2021, Kenya iliagzia bidhaa zenye thamani ya dola milioni 396 kutoka Tanzania ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka  2020 wakati bidhaa zilizoagiziwa zilikuwa na thamani ya dola milioni 347.6.

Viwanda vya Kenya hununua kutoka Tanzania nafaka, mbao, mboga chakula cha wanyama na bidhaa za karatasi.

Takwimu zinaoneysha kuwa katika kipindi hicho bidhaa zilizouzwa Tanzania kutoka Kenya zilikuwa zenye thamani ya dola milioni 267.47 hii ikitajwa kuwa ni mara ya kwanza Tazania kuongoza katika biashara baina ya nchi mbili.

Bandari ya Dar es Salaam

Aghalabu ya bidhaa ambazo Kenya inauza Tanzania ni za kiviwanda kama vile dawa, plastiki na chuma.

Mwezi Septemba Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki Kenya alisema kuna ishara nzuri katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba uhusiano wa Kenya na Tanzania umeimarika sana.

Biashara baina ya pande mbili imeboroka kufuatia mapatano ya mwezi Mei mwaka jana baina ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu kusitisha mizozo ya kibiashara baina ya nchi mbili.

Baada ya kuapishwa mwezi Machi 2021, Rais Samia alitembelea Kenya mwezi Mei kwa lengo la kuimarisha uhusiano baina ya nchi mbili. Katika safari hiyo alisisitiza kuwa lengo lake ni kuhitimisha migogoro ya kibiashara ambayo ilikuwa inavuruga biashara baina ya nchi mbili kwa miaka mingi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments