Recent-Post

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara yasogeza mbele mitanange minne ya Ligi Kuu ya NBC leo

MECHI nne za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara zilizokuwa zichezwe leo zimeahirishwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, wamefikia uamuzi huo kwa sababu timu nne zipo kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi jijini Zanzibar.

Azam FC na Namungo FC pamoja na Simba na Yanga zote zipo kwenye Kombe la Mapinduzi na leo zitakuwa na mechi za Nusu Fainali katika dimba la Amaan jijini Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments