Recent-Post

CCM WATANGAZA MCHAKATO WA KUPATA SPIKA WA BUNGE MPYA.... FOMU KUDAKA KITI CHA NDUGAI ZINAANZA KUTOLEWA KESHO


 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu za kumpata mwanachama atakayewakilisha chama hicho kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania.

Hatua hiyo inakuja baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo Januari 6, 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Januari 9 katika ofisi Kuu za CCM Kisiwandui Zanzibar, Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema mchakato wa kuchukua fomu utaanza Jumatatu Januari 10, 2021 na mwisho wa kurejesha itakuwa Januari 15, 2022.

Post a Comment

0 Comments