CCM YAMPITISHA DKT TULIA KWENYE USPIKA

NI TULIA Ackson! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia jina la Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea nafasi ya uSpika wa Bunge.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama hicho kujadili na kuchambua orodha ya wagombea waliochukua fomu ya kuwania kiti hicho na hivyo kuteua Jina la Naibu Spika huyo.

Shaka amesema hatua inayofuata baada ya Kamati Kuu kufanya maamuzi hayo ni jina la Dkt. Tulia kwenda kupigiwa kura kwenye kikao cha Wabunge wa Chama hicho (Cocas).

Jina la Dkt Tulia limepitishwa baada ya mchujo uliofanyika ambapo wanachama 70 wa wa Chama hicho walichukua fomu ya kugombea nafasi hiyo baada ya aliyekua Spika, Job Ndugai kujiuzulu mapema mwezi huu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments