EAES kuadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Tanzania

Chama cha Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES) kitaadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) mwaka huu hapa Tanzania siku ya Mei 3, 2022.

Huo utakuwa mkutano wa tatu wa kikanda na wa kwanza kufanyika kwa kuwakutanisha pamoja wahariri kutoka nchi mbalimbali.

Akithibitisha kuitishwa kwa kikao hicho leo, Mwenyekiti wa EAES, Churchill Otieno amesema katika taarifa ya EAES kwamba chama hicho kinakusudia kujielekeza zaidi katika masuala ya uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa habari katika kanda hii na kwingineko.

“Tunafuraha kwa kuweza kukutana ana kwa ana na kujadili masuala muhimu yanayovikabili vyombo vya habari katika ukanda huu. Pia, tunaishukuru Tanzania na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa kuonyesha uungwana katika kuandaa mkutano huu,” amesisitiza.

Mwaka huu, kaulimbiu ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ni “Uandishi wa Habari Unaofuatiliwa” na eneo hilo liko hai kwa masuala haya.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile amesema wanatarajia kusherehekea siku hiyo na wafanyakazi wenzao kutoka mikoani na kwingineko.

“Tanzania inafuraha kuwa mwenyeji wa wahariri, waandishi wa habari na wanataaluma wa habari katika ukanda huu. Kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu, chama kikaona ni vyema sio tu kushiriki ana kwa ana ikizingatiwa kuwa ugonjwa wa Uviko-19 unaendelea kuangamiza jamii, lakini pia kutembelea Tanzania.

“Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani inayoadhimishwa nchini Tanzania itaimarisha dhamana ya undugu wa vyombo vya habari kote katika kanda hii,” amebainisha Balile katika taarifa hiyo.

Mwaka jana, chama kilichangia Azimio la Windhoek +30 ambapo masuala ambayo ilijadili na kuwasilishwa Windhoek yalipitishwa.

Katika moyo wa Jumuiya ni kubadilishana mawazo, kujenga mshikamano na mitandao kwa ajili ya kujifunza na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari katika kanda hii.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments