KAMATI YA SIASA WILAYA YA HANANG' YATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO

 

Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja (katikati) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa wa wilaya hiyo wakati wakikagua miradi ya maendeleo.










KAMATI ya Siasa  Wilaya ya Hanang ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  Mathew Dallema wametembelea na kukagua miradi ya afya, Maji, Miundombinu ya Elimu Sekondari na Msingi Barabara, Kilimo na Umwagiliaji yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 5.3.

Miradi mahususi iliyotembelewa ni pamoja na Kikundi cha  Wapambanaji  chenye mradi wa Bodaboda Sh.28,000,000.00 kutoka cha Kata  ya Katesh, Kikundi cha Upendo chenye mradi wa  bakery chenye mtaji wa   Sh. 10,000,000.00 Ujenzi wa madarasa mawili ya fedha za  Uviko 19 Sekondari ya Katesh Sh.10,000,000.00, Kituo cha Afya Mogitu Sh. 550,000,000.00, Barabara ya Ishiponga _ Mirongoli Sh.39,600,000.00 Mradi wa Maji Gidika wenye thamani ya Sh.245,000,000.00 Kituo cha Afya Bassotu Sh.400,000,000.00, Shule Shikizi Laja Tsh 60,000,000.00, Sekondari ya Bassotu Sh.80,000,000.00.

Miradi mingine iliyotembelewa pamoja na Mradi wa Madarasa mawili Ganana Sekondari yenye Sh.40,000,000.00, Madarasa 4 sekondari ya Nangwa yenye thamani ya Tsh 80,000,000.00, ujenzi wa madarasa mawili shule ya Sekondari Saqaderu yenye thamani ya Tsh 40,000,000.00, ujenzi  na upanuzi wa skimu ya umwagiliaji Endagaw Tsh 989,719,851.66 na Mradi wa Maji Kinachere wenye thamani ya Tsh 152,663,491.31.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa niaba ya wajumbe wa Kamati ya Siasa i Mathew Dallema amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi kwa Wilaya ya Hanang na amepongeza Viongozi wa Serikali wa wilaya kwa usimamizi  mzuri na ufuatiliaji unaofanyika katika miradi hiyo  na ameagiza ile ambayo haijakamilika kwa asilimia 100, kasi iongezeke ili wananchi wapate huduma kusudiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi Janeth Mayanja amewashukuru wajumbe wa Kamati ya Siasa wa Chama cha Mapinduzi kwa kutembeleana kufanya ukaguzi wa miradi hiyo na ameahidi kufanyia kazi ushauri uliotolewa  na Wajumbe hao wa kamati ya Siasa wa  Chama cha Mapinduzi ili kuleta tija na masilahi ya Wananchi wa Hanang. 

   Na Mwandishi Wetu


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments