Kenya yakaribisha wawekezaji kutoka Iran katika sekta za mafuta, dawa na vifaa vya tiba

Mwambata wa kiuchumi katika ubalozi wa Kenya mjini Tehran amesema nchi yake inakaribisha wawekezaji kutoka Iran kwenda kuwekeza vitega uchumi katika nchi hiyo.

David Karanja ameyasema hayo katika mkutano wa ustawishaji biashara kati ya Iran na Afrika Mashariki na akabainisha: "tutakuwa na mashirikiano na nchi ya Iran katika bidhaa za mafuta, dawa na vifaa vya matibabu."

Karanja ameongeza kuwa, Kenya ina hamu ya kuvutia fursa za uwekezaji wa pande mbili baina yake na Iran.

Wakati huohuo, Sina Sanjari, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya kimataifa ya tafiti za kiviwanda na kibiashara, na katibu wa mkutano wa ustawishaji biashara kati ya Iran na Afrika Mashariki amesema, lengo la kufanyika mkutano huo ni kujadili changamoto na fursa za uwekezaji na usafirishaji bidhaa za Iran katika eneo la Afrika Mashariki.

Inafaa kukumbusha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewezekeza pia katika sekta za sayansi na teknolojia nchini Kenya kupitia kituo chake cha Ubunifu na Teknolojia (IHIT) kilichoko jijini Nairobi.

 

Balozi wa Iran nchini Kenya Dkt. Jaafar Barmaki (kushoto) akiwa katika Kituo cha Ubunifu na Teknolojia cha Iran (IHIT) mjini Nairobi

Kupitia kituo hicho kilichofunguliwa mwezi Januari mwaka uliopita wa 2021, hadi sasa bidhaa 20 za uga wa sayansi na tekonolojia ambazo zimetengenezwa Iran zimesajiliwa nchini Kenya na zinapatikana katika soko la nchi hiyo na zinaweza kuuzwa pia katika nchi jirani.

Baadhi ya vifaa vilivyosajiliwa ni vile vinavyotumika katika chumba cha wagonjwa mahututi, vipima joto, mavazi maalumu ya hospitali n.k.

Aidha bidhaa zenye thamani ya dola 70 elfu za sayansi na teknolojia zimetumwa huko Kenya tangu kituo cha IHIT kifunguliwe nchini humo.../

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments