Kiongozi wa machinga aipa neno Serikali

Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo wakiwa wanaangalia namna soko la Karume lilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Jumapili Januari 16, 2022.

Msemaji wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Masoud Isa licha ya kulipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kufanya kazi nzuri ya kudhibiti moto uliounguza soko la Karume lakini ameimeomba Serikali kuwatengenezea wafanyabishara miundombinu mizuri itakayowasaidia kukabiliana na ajali kama hizo zisilete madhara makubwa.

Amesema ajali ya moto kutokea kwenye soko hilo la Karume (Mchikichini) ni mara ya tatu na muda wote huo wafanyabishara wamekuwa wakipata hasara kubwa ya mali zao kuteketea kwa moto.

Akizungumza Leo Januari 16, 2022 kwenye soko hilo, Kiongozi huyo ameomba Serikali watengeneze miundombinu wezeshi ikiwemo masinki ya kudumu yasiwe ya kuungua moto huku akimuomba Ras  Samia Suluhu Hassan kusimamia.

"Kutokea majanga kama haya kwenye soko hili sio mara ya kwanza ni mara ya tatu sasa na kipindi chote watu wanapoteza mali zao tunaiomba serikali itutengenezee miundombinu mizuri ya kukabiliana na hili tatizo ikiwemo kujengewa masinki ya kudumu,"amesema Isa

"Kutokea majanga kama haya kwenye soko hili sio mara ya kwanza ni mara ya tatu sasa na kipindi chote watu wanapoteza mali zao tunaiomba Serikali itutengenezee miundombinu mizuri ya kukabiliana na hili tatizo ikiwemo kujengewa masinki ya kudumu,"amesema Isa

Kiongozi huyo amewaomba wamachinga wenzake kuendelea kuwawatulivu wakati serikali inaunda Kamati ya kuchunguza ili kubaini kiini cha tukio hilo.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments