Recent-Post

LOWASSA ALAZWA MUHIMBILI

 

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.‬

‪Taarifa kutoka kwa familia ya Mh Lowassa zinasema kuwa kiongozi huyo amelazwa katika hospitali hiyo kwa karibu wiki nzima baada ya kufanyiwa upasuaji. ‬

‪Akizungumza leo Ijumaa Januari 28, Mbunge wa jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa ambaye ni mtoto wa Lowassa amesema baba yake alilazwa katika hospitali hiyo alipopatwa matatizo ya tumbo.‬

‪"Baba alilazwa kama siku tano zilizopita. Wala haina siri, alifanyiwa upasuaji wa tumbo, lakini bahati mbaya ikaleta complication (hitilafu). Alifanyiwa hapo hapo Muhimbili,”-Fredrick Lowassa‬

‪Amesema wanaomba watanzania, kuendelea kumuombea ili afya yake iendelee kuimarika

Post a Comment

0 Comments