Maandamano hayo yalifanyika katika mji wa Lubumbashi ulioko kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya kushinikiza kuachiliwa huru Daniel Ngoy Mulunda, mkuu wa zamani wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Congo kutoka mikononi mwa wafuasi wa Joseph Kabila, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na ambaye (Mulunda) pia ni mpinzani wa serikali ya hivi sasa ya nchi hiyo.
Maandamano hayo yaliingiliwa kati na polisi ambayo iliyavunja na kupelekea makumi ya watu kujeruhiwa.
Kufuatia ghasia zilizojiri baada ya polisi kuyavunja maandaamano, watu wasiopungua 50 wameripotiwa kujeruhiwa ambapo hali ya watu 14 kati yao inasemekana kuwa mbaya sana.
Waandamanaji wengine 10 wanaripotiwa kutiwa nguvuni na polisi.
Hii ni katika hali ambayo Moise Katumbi, mwanasiasa mashuhuri wa Kongo amelaani hatua ya polisi ya kutumia mabavu kuvunja maandamano hayo yaliyokuwa ya amani. Ngoy Mulunda alikamatwa na kuhukumiwa miaka mitatu jela kwa tuhuma za kuchochea ghasia na kueneza chuki nchini Congo.
0 Comments