Majambazi waua raia 50 nchini Nigeria



Wakazi wanasema makumi ya majambazi waliokuwa wakiendesha pikipiki walivamia kijiji cha Dankade katika jimbo la Kebbi Ijumaa usiku na kufyatuliana risasi na maafisa wa usalama wakiwemo wanajeshi na polisi.

Mashuhuda wanasema maafisa wa usalama walionekana kushindwa nguvu na kurudi nyuma mapema Jumamosi na hivyo kuwapa fursa wanamgambo kutekeleza mauaji sambamba na kupora maduka, nyumba, maghala ya nafaka na pia kuiba mifugo.

Inadokezwa kuwa raia 50 waliuawa katika hujuma hiyo na hali kadhalika pia  wanajeshi wawili waliuawa na majambazo hao ambapo pia waliwateka nyara wanakijiji wengi hasa wanawake na watoto na pia mkuu wa kijiji.

Didzi Umar Bunu, mwanae mkuu wa kijiji amesema majambazi walirejea mapema Jumapili na kuteketeza moto nyumba kadhaa.

Mashambulizi hayo yamejiri wiki moja baada ya zaidi ya watu wengine 200 kuuawa katika hujuma ya majambazi katika jimbo la Zamfara, kaskazini magahribi mwa Nigeria.

         

          

Taarifa zinasema watu 18 wameuawa katika shambulizi dhidi ya jamii ya Ncha, katika sehemu ya Bassa, jimbo la Plateau, huku watu wengine 34 wakiuawa katika sehemu za Nakuna na Wurukuchi, jimbo la Niger.

Tukio katika jimbo la Niger limeonekana kuwa la kulipiza kisasi, baada ya kutokea mauaji wiki chache zilizopita pale wapiganaji wa kijamii katika eneo hilo kuua watu kadhaa waliokuwa wamejihami kwa silaha na waliokuwa wanashutumiwa kwa kuwahangaisha raia.

Wiki iliyopita Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aliahidi kuwa serikali haitalegea katika vita vyake dhidi ya majambazi wanaowahangaisha wananchi.

Maeneo ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa Nigeria yamekuwa yakishuhudia ongezeko kubwa la vitendo vya uhalifu huku serikali ikiwa mbioni kurejesha amani bila mafanikio. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments