Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika ataka maelezo baada ya mkanyagano ulioua mashabiki Cameroon

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe, ametaka maelezo kuhusiana na tukio la msongamano wa mashabiki wa soka uliopelekea watuu kadhaa kupoteza maisha nchini Cameroon.

Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika amesema hayo siku moja baada ya mkanyagano uliosababisha vifo vya takriban watu wanane kwenye uwanja wa Olembé kabla ya mechi ya AFCON kuanza. Kiongozi huyo ametangaza hatua kadhaa na kuomba ripoti ya haraka kuhusu mkasa huo.

Akizungumza baada ya kuwatembelea majeruhi wa tukio hilo waliolazwa hospitalini, Patrice Motsepe amezungumza na waandishi wa habari ambapo alianza kwa kukaa kimya kwa muda wa dakika moja kabla ya kutuma rambirambi zake kwa familia zilizopoteza wapendwa wao siku Jumatatu katika mkasa huo.

                                       

Kiongozi huyo wa CAF, kutoka Afrika Kusini ametangaza hatua ya kwanza muhimu: hakutakuwa na robo fainali katika uwanja wa Olembé siku ya Jumapili, Januari 30. Mechi hii, ambayo itakutanisha mshindi kati ya Côte d'Ivoire na Misri dhidi ya mshindi kati Morocco na Malawi, imehamishiwa kwenye uwanja wa Ahmadou-Ahidjo huko Yaoundé.

Tukio hilo la msongano uliopelekea watu wanane kuaga dunia na ambalo limewahuzunisha mashabiki wa soka kote dunianii lilitokea wakati wa mechi ya kandanda kati ya timu ya taifa ya Cameroon, mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na timu ya taifa ya Comoro. Picha za video zinaonyesha mashabiki waking'ang'ana kuingia kwa nguvu katika uwanja Paul Biya uliopo katika mji mkuu, Yaounde.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments