MLINZI ASEMA MATEJA NDIYO CHANZO CHA SOKO LA KARUME KUTEKETEA KWA MOTO

KUFUATIA tukio la usiku wa kuamkia Jumapili, Januari 16, 2022 la soko la wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Machinga maeneo ya Mchikichini Jijini Dar es Salaam kuteketea kwa moto kwa zaidi ya asilimia 85 na kuacha sehemu kubwa ya soko hilo likiwa majivu matupu.

Mmoja wa walinzi wa soko hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Thomas Benedicto, ameeleza chanzo kamili chamoto huo kupitia mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini na kusema kuwa chanzo kikuu cha moto huo ni Mateja waliokuwa wakitengeneza mihadarati kwa kutumia mshumaa ambao ulidondoka na kuanza kuunguza banda walilokuwa wamekaa.

Wakati moto unaanza nilikuwepo mimi ni moja ya Walinzi wa siku hiyo, sikuwa mbali na banda lililoanza kuungua niliitwa na kwenda kuanza kupambana kuzima moto, ilibidi tukate bomba la choo cha Halmashauri na kuchukua ndoo za choo hicho ili kuweza kuuzima moto japo ulituzidi nguvu.

Chanzo cha moto ni Mateja ambao tupo nao sokoni Karume, wao wanajihusisha na kuuza viatu, pale sokoni kuna moja ya banda ambalo wao wanalitumia kutengeneza mihadarati yao ambayo huwa wanatumia mishumaa kuitengeneza, siku hiyo mshumaa ulianguka na kuanza kuungua,” amesema Thomas.

Matukio ya masoko makubwa hapa nchini kuwaka moto yameshamiri kiasi cha kuibua minongono mingi miongoni mwa watu ambao wengi wamekuwa wakihoji juu ya ufumbuzi wa suala hilo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments