Recent-Post

NAIBU SIPA WA BUNGE AJIUZULU KWA KUDHALILISHWA

Naibu Rais wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo kutokana na kile alichokitaja kuwa udhalilishaji na ukandamizaji.

Jean-Marc Kabund ambaye ni mpambe wa karibu wa Rais Felix Tshisekedi wa DRC alijiuzulu jana Ijumaa, siku mbili baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kanda ya video ya kamera ya CCTV, ikionesha askari wa Gadi ya Rais wakivamia makazi ya Naibu Spika huyo wa Bunge la nchi.

Wasemaji wa serikali na Gadi ya Rais, ambalo ni tawi la jeshi la nchi hiyo ya katikati mwa Afrika, hawajatoa taarifa kuhusu tukio hilo la kushambuliwa makazi ya Kabund, ambapo mtu mmoja alikamatwa.
 Rais Felix Tshisekedi wa DRC

Video hiyo ya CCTV inaonesha namna askari hao waliokuwa wamevalia magwanda ya kijeshi walivamia nyumba ya Kabund, mwendo wa saa moja na nusu magharibi Jumatano, na kumchukua mtu mmoja kwa nguvu, huku wakimpiga mateke.

Naibu Rais wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kujiuzulu kwake kunafungua ukurasa mpya wa historia ya nchi hiyo, katika jitihada za kukabiliana na ukandamizaji, utesaji na udhalilishaji.

Post a Comment

0 Comments