RAIS SAMIA : ATAKAYESUMBUA NI SHATI LA KIJANI SIYO MPINZANI

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na kile alichokisema Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu Serikali kukopakopa badala ya kujiendesha kwa pesa za ndani.

Samia amesema hayo wakati akipokea ripoti ya matumizi ya Fedha za Maendeleo (Fedha za Uviko-19), Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Mtu mmoja aliniambia, atakayekusumbua kwenye uongozi wako ni shati ya kijani mwenzio (yaani Mwana-CCM) na sio mpinzani, mpinzani atakutazama unafanya nini, ukimaliza hoja zao hawana maneno, anayetazama mbele 2025 huyu ndiyo atakayekusumbua ndicho kinachotokea.


“Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025.

“Wakati mmenikabidhi huu mzigo, nilianza kusikia lugha zinasema serikali ya mpito, serikali ya mpito Bungeni huko kwa kina Kassim, nikarudi kwenye Katiba kuangalia serikali ya mpito imeandikwa wapi, sikuona, nikasema anhaa, twendeni,” Rais Samia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments