Recent-Post

Rais Samia kufumua Baraza la Mawaziri

Rais Samia Suluhu Hassan amesema baada ya kukaa kwenye nafasi hiyo miezi nane, anategemea kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni.

Rais Samia amedokeza hayo leo Jumanne Januari 4, 2021 Ikulu ya Dar es Salaam Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 akisema nchi imekuwa ikikopa tangu uhuru lakini haijawahi kupata mkopo nafuu kama huu.

Amesema kuwa baada ya kuwasoma kwa muda, sasa anatarajia kutoa orodha mpya ya wateule ambao anaona watamsaidia kuwaletea wananchi maendeleo.

“Nimeweka watu ninaoamini mtanisaidia kazi, wakuu wa mikoa nimekuwekeni nikiamini kule nilikowakasimia madaraka mtakwenda kusimamia kazi nawengine wote makatibu wakuu na mawaziri” amesema

“Nimekaa nadhani huu ni mwezi wangu wa nane sijui, nilisema nilikuwa nawasoma nanyi mnanisoma, na siku niliyofanya mageuzi ya mawaziri kidogo nikasema hapa nimeweka koma, kazi inaendelea”

Nataka niwaambie nitatoa listi mpya hivi karibuni, wale wote ninaohisi wanaweza kwenda na mimi nitakwenda nao” amedokeza mkuu huyo wa nchi


 

Post a Comment

0 Comments