Sengerema mguu sawa kuelekea uchaguzi CCM

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, Marco Makoye amewataka viongozi wa chama hicho kuwa waadilifu kuelekea uchaguzi ndani ya chama ili kupata viongozi bora.

Kauli hiyo ameitoa kwenye semina elekezi ya makatibu wa CCM kata ya Jumuiya zote iliyofanyika Januari 7, 2022 wilayani humo lengo likiwa kujipanga uchaguzi ndani ya chama hicho.

Amesema uchanguzi ndani ya chama unatarajia kuanzia machi mwaka huu ambapo wataanza na ngazi ya mashina huku amewataka vijina kujitokeza kuwania nafasi hizo ili wakisaidia chama kushika hatamu.

"Kwa sasa vijana nguzo nguzo ya Taifa hivyo wanatakiwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama" amesema Makoye.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Sengerema, Muhsin Zikatimu amesema atahakisha chama kinapata viongozi bora ambao watachaguliwa na wanaCCM kwa kufuata misingi ya chama hicho.

Amewaonya ambao wameanza kupanga safu za uongozi kuanzia ngazi ya mashina kuwa chama hakina utaratibu wa kupanga safu hivyo wanatakiwa kuacha dhana hivyo na chama hakitamvumilia mtu yoyote ambaye atabainika kupanga safu za uongozi ndani ya chama hicho.

Safu za uongozi zinatuchelewesha hivyo lazima tuachane na dhana hivyo ili tufikie malengo yetu ya kuendelea kuongoza nchi" amesema Zikatimu.

Baadhi wa makatibu waliohudhuria semina hiyo, Hilali Lusule amesema wamejengwa na kujengeka hivyo watafuata misingi waliyopewa ili  kuwapatia viongozi bora watakao kisaidia chama kuendelea kushika dora.

Post a Comment

0 Comments