Recent-Post

SIMBA SC YAMTANGAZA AHMED ALLY AFISA MAWASILIANO WAO MPYA

 

                 NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


KLABU ya Simba SC imemtambulisha Ahmed Ally kuwa ndio meneja mawasiliano wa klabu hiyo baada ya nafasi hiyo kukaa muda mrefu bila mtu mara baada ya kuondoka Haji Manara kutimkia kwa mahasimu wao Yanga hivi karibuni.

Ahmed Ally kabla ya nafasi hiyo amewahi kufanya kazi Sahara Media (Star TV & Radio Free) pamoja na Azam Media kabla ya leo kutangazwa Simba Sc.

Kwenye kurasa za mitandao ya kijamii Simba Sc imeandika "Ni kijana mchapakazi, mwenye uhusiano mzuri na watu wa aina zote, mtanashati na kubwa zaidi mapenzi yake kwa Simba hayapimiki".

Post a Comment

0 Comments