THBUB yalaani mauaji nchini, yataja sababu tano

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imelaani mauaji yaliyoripotiwa katika siku za hivi karibuni huku ikitaja sababu ambazo imedai zimesababisha mauaji hayo.

Akizungumza leo Ijumaa Januari 28, 2022 Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ametaja sababu tano ambazo amedai kuwa zinazosababisha mauaji hayo.

Sababu alizotaja Jaji Mwaimu ni pamoja na ulipaji wa visasi, ushirikina, kutozingatia sheria, watu kujichukulia sheria mkononi na sababu kuu ni watu kutokuwa na imani na vyombo vya maamuzi.

Katika siku za hivi karibuni kumeibuka mauaji ya mfululizo kwa watu ikiwamo tukio la hivi karibuni la mauaji ya familia ya watu 5 katika Kijiji cha Zanka Wilaya ya Bahi.

Jaji Mstaafu amesema huu ni wakati Kwa Serikali za mitaa kupitia kwa wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji kurudisha jamii kwenye misingi ya uaminifu.

"Lakini tukubali kurudi kwa viongozi wa dini kwani wao wakisema mambo mengi kwa jamii husikilizwa na kuaminiwa kuliko makundi mengine," amesema Jaji Mwaimu.


 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments