Ukarabati Jengo La Jumuiya Ya Wazazi Dodoma Wakamilika


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Dkt. Edmund Mndolwa akionyesha ufunguo juu kama ishara ya kupokea jengo la Jumuiya hiyo lililopo katika eneo la Mji Mpya Dodoma mara baada ya kukamilika kwa ukarabati uliokuwa ukifanywa na Kampuni ya Jitegemee Trading Company Limited.(Picha na CCM Makao Makuu)


Jumuiya ya Wazazi leo imekabidhiwa jengo lake lililopo katika eneo la Mji Mpya Dodoma mara baada ya kukamilika kwa ukarabati uliokuwa ukifanywa na Kampuni ya Jitegemee Trading Company Limited.


Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Dkt. Edmund Mndolwa amesema kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia sana kurahisisha utendaji wa Jumuiya hiyo, pia ametoa shukrani zake za dhati kwa Chama Cha Mapinduzi hususani Katibu Mkuu Ndugu Daniel Chongolo.

“Nichukue fursa hii kushukuru Chama Cha Mapinduzi hususani Katibu Mkuu Bwana Chongolo kwa ushirikiano aliotuonyesha”.

Dkt. Mndolwa pia alieleza kuwa uzinduzi rasmi wa jengo hilo utatangazwa na mgeni rasmi wa uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Awali akitoa maelezo ya ukarabati wa jengo hilo ambalo lilikuwa la ghorofa moja, Meneja wa Kampuni ya Jitegemee Ndugu Zainabu Juma alisema gharama kuu za ukarabati huo ni Tshs. 230,806,705.

Viongozi mbali mbali walishiriki makabidhiano hayo akiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Bw. Gilbert Kalima, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya (Zanziba) Ndg. Othman Maulid, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Jitegemee Ndugu Martha Uleka, Walimu Wakuu wa Shule za Jumiya pamoja na Viongozi nawadau wengine mbalimbali.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments