Vita sasa kuhamia nafasi ya Naibu Spika


 Kuteuliwa kwa Dk Tulia Ackson kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania uspika wa Bunge la Tanzania kunahamishia vita kwenye nafasi ya unaibu Spika.

Kutokana na wingi wa wabunge wa CCM ndani ya Bunge la 12, linamhakikishia Dk Tulia kutokuwa na kipingamizi cha kuukwaa uspika na kuacha vumbi kuanza kutimka kumtafuta mrithi wake ili kujaza nafasi.

Akizungumza jijini Dodoma jana baada ya kupitisha jina la Dk Tulia, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alisema jina la atakayegombea nafasi ya Naibu Spika litatajwa baadaye.

Lakini, inaelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa wabunge watakaochukua fomu kuwania kiti hicho kuwa wengi kama ilivyokuwa kwenye nafasi ya uspika.

Ibara za 85 na 86 za Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 zimezungumzia uchaguzi wa Naibu Spika na kufafanua mazingira ambayo yakitokea basi uchaguzi wa Naibu Spika unaweza kufanyika kwa kupiga kura ya siri.

Ibara ya 85.1 ya Katiba inasema “Kutakuwa na Naibu wa Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na wajumbe kutoka miongoni mwa Wabunge.”

Ibara ya 86 inasema uchaguzi wa Naibu wa Spika, utafanywa kwa kura ya siri na utaendeshwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

Soma zaidi gazeti la Mwananchi leo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments