Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Januari 13, 2022

RANKA ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Januari 13, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 146.45 na kuuzwa kwa shilingi 147.85 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.2 na kuuzwa kwa shilingi 20.4.

Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.205.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.41 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.28.

Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3104.5 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3135.8.

Kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2588.91 na kuuzwa kwa shilingi 2615.03.

Wakati huo huo,Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 358.734 huku ikiuzwa kwa shilingi 362.29 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 19.85 na kuuzwa kwa shilingi 20.04.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments