Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Januari 21, 2022

 FRANKA ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206.


Dola ya Marekani nchini inanunuliwa kwa Shilingi 2285.515 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.38.

Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2592.223 na kuuzwa kwa shilingi 2618.375.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Januari 21, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3112.175 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3144.223.

Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 360.382 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.95 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 20.0133 na kuuzwa kwa shilingi 20.212.

Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.655.
Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 150.35 na kuuzwa kwa shilingi 151.77 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.15 na kuuzwa kwa shilingi 20.32.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments