WAANDISHI WA HABARI KADHAA MKOA WA MWANZA WAFARIKI DUNIANI KWA AJALI YA GARI

 

"Gari la waandishi wetu wa Mkoa wa Mwanza lililokuwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega lilikuwa linaelekea Ukerewe kwa kupitia Bunda.

Hayo yamebainishwa leo Januari 11, 2022 na Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Mwanza.

"Nineongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ndugu Gabriel (Mhandisi Robert Gabriel) amethibitisha kupokea taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki.Majina ya wenzetu hao tutayatoa kadri tutakavyofuatilia.

Kwa sasa Mkuu wa Mkoa nae anaelekea eneo la tukio nasi pia tunajipanga kwenda eneo la tukio.Naomba tuwe watulivu kwa wakati huu, wakati team yetu na ya Mkuu wa Mkoa tunafuatilia tukio hilo,"amefafanua Soko.
NA MWANDISHI MAALUM

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments