Wabunge CCM wampitisha Dk Tulia kugombea uspika

Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson akiwashikuru wabunge wa CCM baada ya kumpitisha kwa kauli moja kuwa mgombea wa kiti cha Spika wa Bunge, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

 Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamempitisha Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuwa mgombea nafasi ya Spika wa Bunge kupitia chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika kesho Jumanne Februari Mosi bungeni jijini Dodoma.

Shughuli ya upigaji kura iliendeshwa kwa wabunge kupiga kura za ndio na hapana baada ushauri uliotolewa na Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde kukubaliwa na wabunge.

Mwenyekiti wa kamati ya wabunge wa CCM, Kassim Majaliwa amesema idadi ya wabunge walipiga kura walikuwa 340.

Dk Tulia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini, alipitishwa kuwania nafasi hiyo na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Januari 20, 2022, hivyo kuwa mgombea pekee wa chama hicho kuwania kiti cha Spika kilichoachwa wazi na Job Ndugai aliyejiuluzu Januari 6, 2022.

Dk Tulia alikuwa akishindana na wagombea wengine 69 ndani ya CCM walioomba kupitishwa na chama chao kuwania nafasi ya kiti hicho.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments