Recent-Post

WANANCHI PELEKENI WATOTO SHULE IKUNGI MAMA SAMIA KAMALIZA KAZI YA MADARASA

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Singida Mhe Jerry C. Muro amewahimiza wananchi wenye watoto wanaopaswa kwenda shule wapeleke watoto shuleni kufuata kuanza kwa muhula mpya wa masomo 2022

                       
Dc Muro ametoa rai hiyo wakati wa ziara ya kamati ya siasa CCM Mkoa wakikagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Ikungi yakiwemo madarasa mapya yaliyoanza kutumika katika muhula mpya wa masomo tangu Tarehe 17/01/2022

Dc Muro amesema wananchi wanapaswa kumuunga mkono Mhe Rais Samia Sulluh Hassan kwa kupeleka watoto shule ili madarasa yaliyojengwa kwa nguvu yake yaweze kuleta tija katika maisha ya wananchi.

                       

Post a Comment

0 Comments